advertise with us

ADVERTISE HERE

KOMBINESHENI YA RASHFORD NA MARTIAL YAZIDI KUNOGA MANCHESTER UNITED


Klabu ya Manchester United imeendeleza wimbi la kutopoteza mchezo wake wa 19 mfululizo baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Crystal Palace.Rashford alikuwa wa kwanza kufunga bao la kuongoza dakika ya 45+1 huku Antony Martial akifunga bao la pili dakika ya 78.

Matokeo hayo yanaifanya Manchester United isalie nafasi ya 5 ikiwa na pointi 62 sawa na Leicester City waliopo nafasi ya nne huku wakiachwa pointi moja na Chelsea waliopo nafasi ya 3 .

Kombinesheni ya Rashford na Martial

Kombinesheni ya wachezaji hawa wawili imekuwa mwiba kwa timu pinzani msimu huu baada ya nyota hao wawili kufunga jumla ya mabao 34 kwenye EPL huku kila mmoja akifunga mabao 17.Nyota hawa wote wameingia top five ya wafungaji bora na jambo la kufurahisha zaidi ni kwamba Rashford ametengeneza mabao 7 huku Martial akitengeneza mabao 5.

Post a Comment

0 Comments