KOCHA SIMBA ATOA SIRI WALIZOTUMIA KUIBOMOA YANGA


Kocha mkuu wa Simba bw. Sven Vandenbroeck amekimwagia sifa kikosi kwa kutoa dozi nzito kwa Yanga katika mchezo wa nusu fainali ya pili ya Azam Sports Federation Cup u liopigwa jana uwanja wa Taifa.
Simba iliichakwaza Yanga kwa mabao 4-1 na kumetinga fainali ya michuano hiyo ambayo watakutana k na Namungo FC katika uwanja wa Nelson Mandela, Sumbawanga mkoani Rukwa, Agosti 2.
Sven amesema katika mchezo wa jana timu ilicheza vizuri na wachezaji walitimiza majukumu yao uwanjani na ndicho kimepelekea kupata ushindi huo mnono na kuleta furaha kwa Wana Simba wote. "Nimefurahishwa na jinsi ambavyo wachezaji wangu walivyocheza walijituma na walitimiza wajibu wao uwanjani kingine ni ushindi mnono tuliopata katika mchezo wa Derby sio jambo dogo hili nawapongeza sana wachezaji wangu," amesema kocha Sven. Kocha amesema amewapa mapumziko ya siku tatu na wataanza mazoezi ya kujiandaa na mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mbao FC utakaopigwa uwanja wa Taifa siku ya Alhamisi.

Post a Comment

0 Comments