BETI NASI UTAJIRIKE

KOCHA NAMUNGO ATOA NENO KUELEKEA MCHEZO WA FAINALI NA SIMBA


Klabu ya Namungo FC imesema kuwa ina kazi kubwa ya kupambana na Simba kwenye mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho unaotarajiwa kuchezwa Agosti 2, Uwanja wa Nelson Mandela Sumbawanga.

Namungo FC ilitinga hatua ya fainali baada ya kushinda bao 1-0 mbele ya Sahare All Stars uliochezwa Julai 11, Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.Namungo watachuana na  Simba ambao walifuvu hatua hiyo baada ya kuicharaza Yanga kwa mabao 4-1 


Kocha Mkuu wa Namungo FC,  Hitimana Thiery amesema kuwa anatambua kuwa kuna kazi kubwa kupambana na mabingwa kwenye mchezo wao wa fainali. 

"Sio kazi nyepesi kushinda mbele ya mabingwa ambao wapo vizuri na tunawaheshimu kwa kuwa tunawatambua vizuri wapinzani wetu na wanajua kile wanachokifanya. 

" Nilikuwepo uwanjani kuona namna ambavyo walikuwa wakipambana ndani ya uwanja, ila hilo halinipi presha nitakiandaa kikosi kipate ushindi, " amesema.

Post a Comment

0 Comments