Kocha Mkuu wa Dodoma FC Mbwana Makata ameweka wazi kuwa atabakia na asilimia kubwa ya wachezaji walioipandisha timu hiyo kwa kuwa wana uzoefu na ligi.Makata ameongeza kuwa ikiwa ataongeza nyota wapya hataongeza wengi kwenye kikosi hicho kwa ajili ya kujiandaa na msimu ujao.
Dodoma FC imepanda kushiriki Ligi Kuu Bara baada ya kumaliza wakiwa vinara wa kundi A la Ligi Daraja la Kwanza wakiwa na pointi 51.Makata amesema kuwa haikuwa kazi rahisi kwa timu kufikia malengo hayo kutokana na ushindani mkubwa aliokuwa akiupata kutoka kwa wapinzani jambo lililokuwa likiwapa nguvu wachezaji kupambana.
Makata amesema:
"Tutafanya maboresho kwa ajili ya kuongeza baadhi ya wachezaji lakini sio kwa kiwango kikubwa ambacho tutakifanya kwani hawa waliopo wapo imara na wana uzoefu na ligi katika upambanaji.Kitu kikubwa ni kuendelea kupewa sapoti kutoka kwa wananchi waendelee kuwa nasi baada ya timu kupanda kwa sababu wao ni watu muhimu," amesema.
0 Comments