advertise with us

ADVERTISE HERE

UONGOZI WA YANGA MJITATHMINI ,KWANINI MORRISON NA EYMAEL WANALETA SHIDA?


Kocha Lucy Eymael amekuwa akilalama mara kwa mara kutokana na usumbufu anaokumbana nao kutoka kwa wachezaji ,viongozi na hata mashabiki wa Yanga. Hilo ni moja ya mambo yanayoweza kumfanya kocha akashindwa kufanikisha adhma yake ya kuijenga timu.  Morrison haonekani kambini na anasema amemalizana na Yanga. Vipi kuhusu ile Molinga day

1.SAKATA LA MORRISON
Uongozi wa Yanga ulisema una mkataba na Morrison lakini tangu julai 14 mcchezaji huyo hakuonekana tena kambini kwa Yanga na hajajiunga na timu hiyo mpaka kesho huku akionekana mitaa mbalimbali akicheza soka la mchangani.Kwa madai ya Morrison ni kuwa hana mkataba na klabu hiyo na mikataba yake ya miezi sita ilikwisha malizika swali linakuja hapa je Uongozi Yanga unamdanganya nani?

2.SAKATA LA MOLINGA 

Unalikumbuka sakata la kocha msaidizi wa Yanga Mkwasa na Molinga ? unakumbuka mchezaji huyo alivyogoma kusafiri na timu kwenda kucheza na mwadui pale shinyanga na mwisho wa siku ikalazimika mchezaji kumkatia tiketi mchezaji huyo ili aweze kusafiri kwa ndege tofauti na wachezaji wenzake swali linakujahapa je Uongozi wa Yanga na wachezaji wao uko vipi

3. SAKATA LA EYMAEL

Hivi karibuni kocha Luc Eymael alinukuliwa akisema Nafanya kazi mazingira magumu sana, mazingira yaliyojaa ubabaishaji mkubwa , sifurahii maisha yangu hapa najiona sina mamlaka yoyote kama kocha mkuu. . naishi na mke wangu nyumba haina hata DSTV. . Timu ina presha kubwa , tunacheza mbele ya mashabiki wetu ambao ni wajuaji wakati hawana uelewa wowote wa mpira. . Yikpe ni mchezaji ambaye anajituma na kujitolea kwa bidii zote na uwezo wake wote kwa ajili ya klabu lakini cha ajabu mashabiki wake wanamzomea wanapiga kelele kama nyani Blaaa blaaah, Nilifanya Sub ya kumtoa kiungo nikaongeza striker bado wanapiga kelele kama nyani wakati hawajui chochote kuhusu soka. . unapocheza ugenini lazima ujue namna ya kupata matokeo . .Nawaachia timu yenu mbaki na mashabiki wenu kwa maaana kwa mwenendo huu hatuwezi kutwaa taji lolote. .Niacheni na maisha yangu nanyi mbaki na timu yenu"
Je Uongozi wa Yanga wanaishije na Kocha huyuPost a Comment

0 Comments