KAGERA SUGAR KUMKOSA MSHAMBULIAJI WAO HATARI ANAYEIJULIA YANGA


Mshambuliaji namba moja ndani ya kikosi cha Kagera Sugar Yusuph Mhilu  ambaye aliitungua Yanga kwenye mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Uhuru, Januari 15 kuna hatihati ya kuikosa Yanga.
Mhilu mwenye mabao 13 alifunga moja ya bao kwenye ushindi wa mabao 3-0 walioupata Kagera Sugar kwenye mechi ya kwanza ya Kocha Mkuu, Luc Eymael kukaa kwenye benchi akipokea mikoba ya Mwinyi Zahera.
, Mhilu amesema kuwa bado hajajua kama anaweza kucheza kwenye mchezo dhidi ya Yanga kwa kuwa ana maumivu ya misuli ya nyama za paja.
Kwenye mchezo wetu dhidi ya Ruvu Shooting uliochezwa Uwanja wa Kaitaba sikumaliza dakika 90 kwa kuwa nilikuwa nina maumivu ya misuli ya nyama za paja, ila kwa sasa ninaendelea vizuri,” amesema Mhilu mwenye mabao 13 na pasi tatu za mabao. 
Yanga itakutana na Kagera Sugar Uwanja wa Kaitaba ikiwa na kumbukumbu ya kulazimisha sare ya bila kufungana na Biashara United kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa jana,Julai 5 Uwanja wa Karume.

Post a Comment

0 Comments