BETI NASI UTAJIRIKE

JUVENTUS YAENDELEZA VIPIGO RONALDO AKITUPIA


Mshambuliaji wa Juventus Cristiano Ronaldo ameendelea kutikisa nyavu za wapinzani wa juventus kuelekea mbio za ubingwa. Mchezo wa 29 uliowakutanisha Juventus na Genoa ulimalizika kwa Juve kushinda mabao 3-1 .

Paul Dybala alikuwa wa kwanza kufungua nyavu za Genoa kwa kufunga bo dakika ya 50,Ronaldo akipachika bao la pili dakika ya 56 na Douglas Costa akifunga bao la 3 dakika ya 73. Matokeo hayo yanaifanya Juventus kuendelea kuongoza ligi kwa pointi 72 dhidi ya 68 za Lazio.

Cristiano Ronaldo anaendelea kupambana vikali kuwania kiatu cha dhahabu huku akitakiwa  kumfikia Ciro Immobile mwenye mabao 29 yeye( Ronaldo) akiwa na mabao 24.

Kikosi cha Juvetus dhidi ya Genoa  

Szczesny,Cuardrado,De LigtBonnuci,Danillo,Betancur,Pjanic/Matuidi,Rabiot/Olivieri,Ronaldo/Costa,Dybala /Higuan,Bernadeschi/Ramsey.

Post a Comment

0 Comments