BETI NASI UTAJIRIKE

JORDAN JOHN ALIVYOINGAMIZA NAMUNGO FC LEO


Klabu ya Namungo FC imejikuta ikipigwa na mshangao baada ya kukubali kipigo cha mabao 3-0 kutoka kwa Mbao FC. Jordan John alikuwa wa kwanza kuiandikia Mbao FC bao la kuongoza dakika ya 4 tu baada ya mpira kuanza. Jordan alirejea tena langoni kwa Namungo na kuandika bao la pili dakika ya 14 na Abdulahim Segeja alifunga bao la tatu dakika ya 28 ya mchezo huo. 

Mpaka mpira unamalizika Mbao walikuwa mbele kwa mabao 3-0 na kuwafanya wasalie nafasi ya 16 wakiwa na pointi 42 sawa na Mbeya City na Mtibwa Sugar.

Kwa upande wa Namungo wao wanabaki nafasi ya  4 wakiwa na pointi 64 nyuma ya Azam FC wenye pointi 66 na Yanga wenye pointi 69. 

Post a Comment

0 Comments