BETI NASI UTAJIRIKE

JE MORRISON AMEKUJA KUTUONYESHA THAMANI YA MCHEZAJI MKUBWA ?


Unapotaja winga bora kwa Yanga msimu huu basi moja kwa moja uttaja jina la Morrison .Tangu awasili nchini mwezi Januari amekuwa akizungumzwa na kila shabiki wa soka la Tanzania . Kama hukuona zile mbwembwe zake alizozionyesha kwenye mchezo dhidi ya Singida United basi utakuwa ulimwona kwenye mechi dhidi ya Simba akifunga goli maridhawa kabisa kwenye mchezo ule uliomalizika kwa wao kushinda bao 1-0 .

Siku za karibuni mchezaji huyo aliingia utata na klabu yake baada ya kuita waandishi wa habari kambini na kusema hajasaini mkataba mwingine na klabu hiyo jambo lililopelekea sintofahamu ndani ya klabu hiyo huku ikisemekana alifikia hatua ya kuondolewa kwenye kikosi cha mkwasa na kusimamishwa mazoezini.

Jana Morrison amekatiwa tiketi ya ndege  kusafiri peke yake kuelekea mkoani Kagera kuungana na wachezaji wenzaKe kwa ajiri ya  mchezo wa ligi kuu dhidi ya Kagera Sugar mchezo utakaopigwa dimba la Kaitaba siku ya Jumatano

Awali taarifa zilisema mchezaji huyo hakusafiri kuelekea Mkoani Mara kwa ajiri ya mchezo dhidi ya Biashara United na asingekuwepo kwenye mchezo dhidi ya Kagera Sugar huku tetesi zikisema atashiriki kwenye mchezo wa nusu fainali FA dhidi ya Simba  lakini hapo jana alilazimika kusafiri peke yake ili kuongeza nguvu kwa timu hiyo .

Swali ni je Morrison ni mchezaji aliyekuja kuwafundisha viongozi wa soka la Tanzania nini maana ya mchezaji mkubwa au amekuja kuonyesha kuwa kuna wachezaji wakubwa zaidi ya timu. Nitahoji swala hili baada ya mechi ya Nusu fainali FA

Post a Comment

0 Comments