HAJI MANARA ATOA NENO BAADA YA USHINDI DHIDI YA YANGA


Msemaji wa klabu ya Simba Haji Manara ametoa neno lake la kwanza baada ya Simba kuibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Yanga mchezo wa nusu fainali AZAM SPORTS FEDERATION CUP uliopigwa dimba la taifa jijin Dar es salaam.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Haji Manara aliandika
 "Alhamdulillah.Nimeandika weeee nimefuta,,nimeandika weee nimefuta,,,lakini wiki hii mtajuta kunijua.

Kauli hii inadhihirisha shangwe kwa msemaji huyo aliyesema kama Simba ingefungwa na Yanga basi angeachana na uraia wa Tanzania na angehama nchi. Haji Manara alikuwa akiipigia promo mechi hiyo kama mechi ya kisasi kwa Yanga baada ya kucheza mechi mbili na mabingwa hao wa kihistoria na kuambulia pointi 1

Post a Comment

0 Comments