BETI NASI UTAJIRIKE

HABARI NJEMA KWA MASHABIKI WA CRISTIANO RONALDO NA JUVENTUS


Mshambuliaji wa Juventus Cristiano Ronaldo ameendelea kung'ara ligi kuu Italy maarufu kama Serie A. Juventus wakiwa nyumbani walilazimishwa sare ya mabao 2-2 dhidi ya Atlanta kwenye mtanange uliokuwa mgumu kwa pande zote mbili.

Duvan Zapata alikuwa wakwanza kufunga bao dakika y 18 lakini Cristiano alisawazisha kw mkwaju wa penati dakika ya 51.Ruslan aliipa tena Atlanta bao la kuongoza dakika ya 80 lakini Ronaldo alilichomoa kwa mkwaju wa penati dakika ya 90 za mchezo huo.

Matokeo hayo yanawafanya Juventus kuimalika kileleni wakiwa na pointi 76 kwenye michezo 32 waliyocheza wakishinda michezo 24 sare 4 na kufungwa 4. Kwa upande wa Atlanta wao wana wanasalia nafasi ya 3 wakiwa na pointi 67 kwenye mechi 32 walizocheza.

Mshambuliaji Cristiano Ronaldo ameweka rekodi ya kuwa na mabao 28 kwenye michezo 28 ya Serie A aliyocheza msimu huu na kumfanya abakize bao 1 tu kumkuta mshambuliaji wa Lazio Ciro Immobile mwenye mabao 29 msimu huu

Post a Comment

0 Comments