BETI NASI UTAJIRIKE

EYMAEL AYATAJA MAJEMBE MATATU YATAKAYOIKOSA SIMBA


Luc Eymael amesema kuwa ni tatizo kubwa kwake kuwakosa nyota wake watatu ambao ni chaguo lake la kwanza.Yanga itamenyana na Simba, Julai 12 Uwanja wa Taifa huku kukiwa na hatihati ya kukosa huduma za nyota wake hao watatu ambao ni Haruna Niyonzima ambaye anasumbuliwa na kifundo cha mguu, Papy Tshishimbi anahitaji kufanyiwa upasuaji wa goti na Mapinduzi Balama alivunjika mfupa mdogo kwenye mazoezi wakati Yanga ilipokuwa inajiaandaa kuvaana na Ndanda FC.

 Eymael amesema kuwa bado hajajua atafanya nini kwa sasa kutokana na wachezaji wake

 hao kutokuwa kwenye ubora.

Ni tatizo kubwa kwa sasa kutokuwa na Tshishimbi, Niyonzima na Balama, kwangu 

mimi nina amini ni wachezaji muhimu ila sina chaguo la kufanya.

“Ninachokifanya ni kuendelea kuwatazama wachezaji ambao nipo nao pia usiku 

ninafikiria kujua hali zao itakuaje, ila ninadhani kwa Niyonzima inawezekana akaanza kwenye mchezo wetu dhidi ya Simba itategemea hali yake itakuaje,” amesema Eymael. 

Kwenye mchezo wa jana wa ligi uliochezwa Uwanja wa Kaitaba, Eymael alicheza bila ya

 wachezaji hao na alishinda bao 1-0 lililofungwa na Bernard Morrison.


Post a Comment

0 Comments