BETI NASI UTAJIRIKE

EYMAEL AWATAJA NYOTA WATAKAOKOSA MECHI NA MWADUI FC


Kocha Mkuu wa Yanga, Luc Eymael amesema kuwa atakosa huduma ya viungo wake wawili Kwenye mchezo wa leo dhidi ya Mwadui FC wa Ligi Kuu Bara utautakaopigwa Uwanja wa Taifa. 

Eymael amesema atakosa huduma ya Mapinduzi Balama pamoja na Haruna Niyonzima ambao ni majeruhi kwa sasa.

Kocha huyo amesema kuwa hawezi kuzungumza kuhusu ishu ya suala la kiungo wao mshambuliaji Bernard Morrison. 

Ni mchezo mgumu dhidi ya Mwadui FC kwa kuwa wao wana malengo yao nasi pia tuna malengo yetu, ila kikubwa tutaingia kuingia kupambana ili kupata matokeo mazuri.

"Nitakosa huduma ya Balama pamoja na Niyonzima hawa ni majeruhi huku suala la Bernard Morrison hilo Siwezi kulizungumzia lipo juu ya uongozi," amesema. 

Mechi ya kwanza walipokutana Uwanja wa Kambarage,  Yanga ilishinda bao 1-0 na kusepa na pointi tatu jumlajumla.

Yanga ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 67 huku Mwadui FC ikiwa nafasi ya 17 na pointi zake 40 inapambana kutoshuka daraja.

Post a Comment

0 Comments