advertise with us

ADVERTISE HERE

EYMAEL ATANGAZA RASMI VITA MSIMU UJAO


Kocha mkuu wa Yanga Luc ymael ameuzungumzia ushindi walioupata dhidi ya ingida United. Yanga walishinda mabao 3-1 yaliyowewa kimiani na Paul Godfrey,Ngassa na Yikpe n kuwafanya wafikishe pointi 67 huku wakitwaa rasmi nafasi ya pili .

Luc Eymael amenukuliwa akisema "Tumeshinda dhidi ya Singida United japo tumepoteza nafasi nyingi za kutanua ushindi wetu, tatizo la kutotumia nafasi za kufunga tuzipatazo linajulikana na tutalifanyia kazi kama benchi la ufundi.Wachezaji wameingia uwanjani wakiwa hawapo sawa kisaikolojia kwa maana walipoteza fahari yao, pesa na imani kwa mashabiki wao kutokana na matokeo ya mchezo uliopita wa jumapili dhidi ya Simba SC.Haijalishi ukubwa wa kipigo kwa maana Hata tungefungwa 5, 3, 2-1 ama tungefungwa kwa mikwaju ya penati bado uhalisia ungekuwa ule ule kuwa tumetolewa, Man City alifungwa goli 3-1 dhidi ya Liverpool lakini mwezi huu mwanzoni wakalipa kisasi kwa goli 4 - 0. . Huwezi kushinda mara zote ila inapotokea umepoteza unarudi kujipanga na kuhakikisha unashinda mchezo ujao, tutarudi imara zaidi msimu ujao"

Post a Comment

0 Comments