EYMAEL AFUNGUKA GAME 2 ATAKAZOMWEKA MORRISON NJE ,AFUNGUKA MCHEZO NA SIMBAKuna uwezekano mchezaji wa Yanga Benard Morrison akawepo kwenye mchezo wa watani wa jadi utakaopigwa tarehe 12 Julai ikiwa ni mchezo wa nusu fainali kombe la FA. Kocha wa klabu ya Yanga Luc Eymael amefunguka kumalizana na mchezaji huyo lakini hatakuwepo kwenye mchezo dhidi ya Biashara United na ule wa Kagera Sugar. Lakini akasisitiza mchezaji huyo atacheza mchezo wa nusu fainali dhidi ya Simba. Eymael amenukuliwa akisema  

Nimeongea na Morrison kwa muda mrefu sana leo, kwa upande wangu nimemalizana naye na sina kinyongo naye . . ila hatokuwa sehemu ya kikosi kitakachocheza dhidi ya Biashara Utd na endapo nikamhitaji mchezo mwingine wa Kagera Sugar basi ntautaarifu uongozi ndo watamleta. . Kijana katuahidi mengi sana makubwa na kikubwa yupo hapa kuisaidia klabu yake na atalithibitisha hilo siku ya mchezo wa nusu fainali dhidi ya Simba SC, Mengine nawaachia uongozi wao ndo watatolea maelezo "

Post a Comment

0 Comments