advertise with us

ADVERTISE HERE

CRISTIANO RONALDO AISHANGAZA DUNIA KWA REKODI MPYA


Mshambuliaji wa Juventus ameendelea kuwa moto mkali baada ya kuisaidia Juventus kushinda mabao 4-1 dhidi ya Torino. Paulo Dybala alikuwa wa kwanza kufunga bao l kuongoza dakika ya 3 tu bada ya mchezo kuanza Cuadrado aliipa bao la pli dakika ya 29 lakini Andre Baleti wa torino aliipa timu yake bao la kufuta machozo dakika ya 45 kwa mkwaju wa Penati.Mpaka kipindi cha pili Juventus walikuwa mbele kwa mabao 2-1.

Rekodi ya Ronaldo
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi na dakika ya 61 Cristiano ronaldo alifunga bao lake la 25 kwa msimu huu na kumfanya aweke rekodi ya kufunga mabao 25 kwa misimu 11 mfululizo. Bao la faulo ni la kwanza kwa Ronaldo kufunga tangu ajiunge na Juventus huku pia akivunja rekodi ya Omar Siviro aliyoweka msimu wa 1960/61 kwa kufunga mabao 25 ndani ya Serie A.Ronaldo amecheza michezo 26 ya Serie A msimu huu na kufunga mabao 25.

Juve iliibuka na ushindi wa mabao 4-1 na kuuifanya kufikisha pointi 75 kwenye michezo 30 waliyocheza.

Kikosi cha Juventus kilianza na 

Buffon,Cuadrado,De Ligt,Bonnuci,Danillo,Betancur,Pjanic,Rabiot,Ronaldo ,Dybala na Benadeschi


Post a Comment

0 Comments