CHELSEA YAKOMAA NAFASI YA NNE IKISHINDA DHIDI YA WATFORD


Klabu ya Chelsea imelipa kisasi kwa Watford baada ya kufungwa mabao 3-2 na Westham United siku chache zilizopita. Chelsea wakiwa uwanja wa nyumbani Stamford Bridge walikuwa wa kwanza kupata bao la kuongoza kupitia Giroud dakika ya 28 huku Willian akifunga bao la pili dakika ya 43 kwa mkwaju wa penati.

Ross Barkley aliipa Chelsea bao la tatu na kuifanya klabu hiyo kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 .Matokeo hao yanaifanya Chelsea ufikisha pointi 57 kwenye michezo 33 huku ikisalia nafasi ya 4 kwenye msimamo wa ligi hiyo.

Kikosi cha Chelsea 

Arrizabalagga,James,Christensen,Zouma,Azipilicueta,Barkley,Kante,Mount,Willian,Pullisic na Giroud 

Post a Comment

0 Comments