BETI NASI UTAJIRIKE

TFF WAFUNGUKA ISHU NZIMA YA YANGA VS MORRISON


 Kamati ya sheria na hadhi za wachezaji ya TFF imesema hakuna mchezaji yeyote anayecheza ligi kuu Vpl bila mkataba.Hivyo basi Bernard Morrison amesema uongo kuhusu kutokuwa na mkataba na klabu ya Yanga, shauri linaendelea na majibu ya ujumla yatatolewa yakiambatana na adhabu kwa aliyedanganya.

Pia mwenyekiti wa kamati hiyo amesema hata madai ya awali ya Bernard Morrison kudai alicheza bila mkataba katika michezo ya kwanza alipotua Tanzania ni uongo hakuna kitu kama hicho.

 Kuhusu klabu ya Yanga kushtaki kuwa Mchezaji wao Bernard Morrison anarubuniwa na klabu nyingine, mwenyekiti amekiri ni kweli wamepata malalamiko hayo na wanayafanyia kazi.

 Mwisho amesisitiza Mkataba wa awali wa miezi (6) na wa miaka (2) yote imesajiliwa TFF na ni halali inatambulika na Shirikisho.


Post a Comment

0 Comments