Nahodha wa klabu ya Simba John Boko ambao ni Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara mara tatu mfululizo amesema kuwa kikubwa kilichowapa ushindi mapema ni ushirikiano wa wachezaji, benchi la ufundi pamoja na sapoti ya mashabiki. Simba imetwaa taji la ligi msimu wa 2019/20 ikiwa na mechi sita mkononi baada ya kufikisha jumla ya pointi 79 ambazo hazitafikiwa na timu yoyote, kwa sasa ikiwa imecheza mechi 34 ina pointi 81. Jana, Julai 8 ilikabidhiwa Kombe hilo ambalo litakuwa kwenye makabati yao jumla baada ya kumalizana na Namungo FC mchezo wa ligi uliochezwa Uwanja wa Majaliwa na dakika 90 kukamilika kwa sare ya bila kufungana. Bocco amesema:"Ushirikiano mkubwa kuanzia Kwenye benchi la ufundi ambao tunapata wachezaji pamoja na ushirikiano kwa kila mchezaji umechangia kwa kiasi kikubwa kwetu kuweza kutwaa ubingwa mapema. "Sapoti ya mashabiki pia imekuwa ikitupa nguvu katika kufanya yale ambayo tumeweza hivyo haikuwa kazi rahisi kufikia hapa lakini tunamshukuru Mungu." Leo Simba inarejea Dar kutoka Lindi majira ya saa mbili ambapo itaendeleza sherehe za ubingwa kwa kutembea na Kombe kwenye gari la wazi
0 Comments