Mshambuliaji wa Simba Meddie Kagere ameendelea kung'ara baada ya kutwaa tuzo ya mchezaji bora mwezi March mwaka huu huku nahodha wa klabu hiyo John Bocco amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa mwezi Juni wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) msimu wa 2019/20. Bocco ametwaa tuzo hiyo baada ya kuwashinda wenzake Atupele Green wa Biashara United na Martin Kiggi wa Alliance FC alioingia nao fainali. Kagere amefunga mabao 19 msimu huu huku Bocco akifunga jumla ya mabao saba ndani ya Ligi Kuu Bara na timu yao ikitwaa ubingwa wa tatu mfululizo. Bocco ametwaa tuzo hiyo baada ya kufunga mabao 3 kwenye michezo aliyocheza mwezi juni na kuisaidia klabu ya Simba kutwaa ubingwa ikiwa na mechi mkononi
Post a Comment
0
Comments
MERIDIAN BET
EURO 2024
Kuanzia tarehe 14 june to 14 july AMOSPOTIXTRA TEAM itakuwa ujerumani kukuletea michuano ya EURO2024
0 Comments