Klabu ya Barceloa imeendelea kufanya vyema La Liga. Wkiwa ugenini dhidi ya Villa Real waliibuka na ushindi mnono wa mabao 4-1. Pau Torres alifungua nyavu za timu yake kwa kujifunga bao dakika ya 3 ya mchezo kabla Gerrald Moreno kusawazisha dakika ya 14 . Luis Suarez aliipa Barcelona bao la pili dakika ya 20 huku Griezman akifunga bao la 3 dakika ya 45.Mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika Barcelona walikuwa mbele kwa mabao 3-1. Ansu Fati alikamilisha ushidi wa Barcelona kwa bao dakika ya 89 na kufanya mchezo huo kumalizika kwa Barcelona 4-1 Villa Real Barcelona anaendelea kuwa nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi akiwa na pointi 73 nyuma ya Real Madrid mwenye pointi 77 wakicheza michezo 34 kila mmoja
0 Comments