AZAM WAICHAKAZA SINGIDA UNITED ,CHIRWA AKIWEKA REKODI MPYAKlabu ya Azam imerejea nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya ushindi wa 7-0 dhidi ya Singida United mchezo uliopigwa dimba a Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.

Azam FC inayofundishwa na kocha Aristica Cioaba kutoka Romania inafikisha pointi 62 baada ya ushindi huo, sasa ikiwazidi pointi moja, vigogo Yanga SC wanaofuatia nafasi ya tatu baada ya timu zote kucheza mechi 33.  

Mabao ya Azam FC leo yamefungwa na kiungo, Iddi Suleiman ‘Nado’ mawili, David Natley aliyejifunga dakika ya 41 na mshambuliaji wake Mzambia, Obrey Chirwa aliyefunga manne dakika za 44, 55, 56 na 62.

Chirwa anakuwa mshambuliaji wa pili msimu huu kufunga  mabao 4 mechi moja huku Meddie Kagere akiwa mchezaji wa kwanza msimu huu kuifunga Singida United idadi hiyo ya mabao.

Hii ni mara ya kwanza kwa klabu ya Azam kuibuka na ushindi wa mabao 7-0 kwenye michuano ya ligi kuu tangu ilipopanda mwaka 2009.
Matokeo hayo yanaifanya Azam Fc kufikisha poiti 62 kwenye michezo 33 ya ligi kuu Tanzania bara

Post a Comment

0 Comments