BETI NASI UTAJIRIKE

ARSENAL WAICHEZESHEA LIVERPOOL KIPIGO CHA TATU EPL


Klabu ya Liverpool imekubali kipigo cha mabao 2-1 dhidi ya Arsenal. Mchezo huo wa raundi ya 36 ulipigwa dimba la Emirates huku Arsenal wakiwa na sauku ya kuzipata pointi 3 muhimu ili kujisogeza nafasi 6 za juu. 

Sadio Mane alikuwa wa kwanza kuip Liverpool bao la kuongoza dakika 20 ya mchezo huku Lacazzete akisawazisha bao hilo dakika 32 ya mchezo Reiss Nelson aliipa Arsenal bao la pili na kuifanya timu hiyo kumaliza kipindi cha kwanza ikiwa mbele kwa mabao 2-1 .

Kipindi cha pili Arsenal walijiimarisha zaidi na mpaka mwisho wa mchezo vijana wa Arteta wliibuka na ushindi wa mabao 2-1. Ushindi huo unawabakiza Arsenal nafasi ya 9 kwenye msimamo wa ligi.Kwa upande wa Liverpool mchezo huo ulikuwa ni kukamilisha rtiba kwani wameshatwaa ubingwa wa ligi hiyo.

Ikumbukwe msimu wa 2019/20 Liverpool amefungwa na timu tatu tu kwenye michezo 36 waliyocheza. Wamefungwa na Wolves ,Manchester City na Arsenal.Kama watashinda michezo miwili iliyobaki ukiwemo dhidi ya Chelsea basi watafikisha pointi 99. 

Post a Comment

0 Comments