advertise with us

ADVERTISE HERE

YANGA: MORRISON AENDELEA KUKIMBIZA MPAKA MAZOEZINIKlabu ya Yanga imeendelea kujifua vikali kuelekea mechi ya juni 13 dhidi ya Mwadui. Mara baada ya ligi kuu kutangazwa rasmi kurejea klabu hiyo yenye maskani yake mitaa ya Jangwani ilirejea uwanjani kwa mazoezi makali ili kujihakikishia ifanya vizuri zaidi kwenye michezo 11 iliyobaki kwenye ligi . 

Mshambuliaji wa kimataifa kutoka Ghana "Morrison "ameonekana kuifurahia programu ya mwalimu mkwasa na amekuwa akifanya mazoezi makali zaidi kuliko wenzake. Nyota huyo aliyejizolea umaarufu nchini Tanzania mara baada ya kufunga bao muhimu kwenye mechi dhidi ya Simba ameendelea kujizolea umaarufu kwa chenga zake za maudhi kwa wapinzani huku mashabiki wa Yanga wakisema hakuna mchezaji mwenye uwezo kama yeye

Haya hapa mazoezi ya wachezaji Yanga Post a Comment

0 Comments