WERNER NDANI YA CHELSEA: MIFUMO MITATU JINSI YA KUMTUMIA


Klabu ya Chelsea imefanikiwa kuingia mkataba na mshambuliaji wa kijerumani Timo Werner akitokea RB Leipzig kwa dau la paundi milioni 47.Mchezaji huyo anaingia klabuni hapo kama mfalme kutokana na rekodi nzuri ya ufungaji aliyoiweka msimu huu baada ya kufunga mabao 32 na kusaidia mengine 13 kupatikana ndani ya klabu kwenye michezo 43 aliyocheza.

Bado mkataba wa mshambuliaji huyo haujawekwa wazi ili inaaminika ataitumikia klabu hiyo mpaka mwaka 2025. Chelsea wanaonekana kujiandaa vyema kwa msimu wa 2020/21 baada ya kumsajili Pulisic,Ziyech na sasa werner na kuwafanya kuwa na safu hatari zaidi ya ushambuliaji.

Mifumo inayoweza kutumiwa na Kocha Lampard

1) 4-3-3  Kepa; James, Christensen, Rudiger, Alonso; Jorginho, Kante, Kovacic; Pulisic, Werner, Ziyech.

Huu ni mfumo uliotumiwa na chelsea kwa msimu wa 2019/20 na kuisaidia klabu hiyo kupata mabao 51 kwenye mechi 29 walizocheza huku Tammy Abraham akiwa mfungaji tegemezi akifunga mabao 13 . Mfumo huu umekuwa tatizo kwa Ngolo Kante na mara nyingi amekuwa akishidwa kweda na staili ya Lampard labda kwa kuwa sababu ya majeraha au kukosa msaidizi.

2) 4-2-3-1 Kepa; James, Christensen, Rudiger, Alonso; Jorginho, Kovacic; Hudson-Odoi, Mount, Ziyech; Werner.

HHuu ni mfumo mzuri kwa Werner kutokana na kuzungukwa na mafundi wengi. Werner atazungukwa na Ziyech(kulia) ,Mount (kushoto) na nyuma yake Hudson Odoi naamini atapata aina mbalimbali za pasi kwa ajili ya kufunga .

3) 3-4-3: Kepa; Azpilicueta, Rudiger, Christensen; James, Jorginho, Kovacic, Alonso; Werner, Abraham, Ziyech

Huu ni mfumo wenye kushambulia zaidi ,Werner ,Abraham,Ziyech wote ni wafungaji wazuri binafsi naona utatengeneza ubinafsi kwa wachezaji hawa na mwisho wa siku washindwe kufanya walichotumwa na mwalimu. Ziyech atataka awe kinara wa ufungaji,Abraham pia na Werner ndiye straika wa mwisho 

Je mfumo upi utaifaa chelsea kwa msimu ujao?

Post a Comment

0 Comments