BETI NASI UTAJIRIKE

WAZIRI MWAKYEMBE AKERWA NA MASHABIKI MBEYA CITY


Waziri wa Habari, Sanaa, Michezo na Utamaduni Dkt Harrison Mwakyembe amesema kuwa kwa kosa la mashabiki wa Mbeya City na Simba kutofuata muongozo wa mita moja itachukuliwa hatua.

 Mbeya City ilikuwa na kibarua cha kumenyana na Klabu ya Simba, mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Sokoine ambapo wamepoteza kwa kufungwa mabao 2-0.

Kwenye mchezo huo mashabiki walijitokeza kwa wingi huku wakisahau kufuata muongozo uliotolewa na Serikali kwa kukaa umbali wa mita moja ili kujilinda dhidi ya Virusi vya Corona.

Timu ya kwanza ambayo ilikutana na rugu la Serikali ni JKT Tanzania ambayo ilifanya hivyo Juni 17 ilipomenyana na Yanga kwenye sare ya kufungana bao 1-1.

Mbeya City imefanya hivyo jambo ambalo Serikali imesema kuwa itachukua hatua katika hili.
Lengo kubwa ambalo linafanywa na Serikali ni kulinda afya za mashabiki na watanzania kiujumla.

Post a Comment

0 Comments