advertise with us

ADVERTISE HERE

TETESI ZA SOKA DUNIANI LEO JUMAPILI TAREHE 21-06-2020

Kandarasi ya mlinzi wa Brazil David Luiz na timu ya Arsenal inamalizika Juni 30 na wasimamizi wake wanasema hatma ya mchezaji huyo, 33, katika klabu hiyo itajulikana mwisho wa wiki. (Talksport)

Luiz anataka mkataba wa miaka miwili kuendelea kuwa na Gunners lakini timu hiyo iko tayari kumuongezea mkataba wa miezi 12. (Mail)

Haki miliki ya pichaBBC SPORT

Chelsea iko tayari kumuuza kiungo wa kati wa Ufaransa N'Golo Kante, 29, kusaidia kukusanya pesa za uhamisho zaidi kufuatia makubaliano ya kumsajili mshambuliaji wa Ujerumani Timo Werner kutoka RB Leipzig. (Times - subscription required)

Matumaini ya Chelsea ya kumsajili kiungo wa kati Kai Havertz huenda yakaimarika zaidi baada ya Bayern Munich na Real Madrid kujiondoa kwenye kinyanganyiro cha kumsajili mchezaji huyo, 21, wa Ujerumani. (Express)

Arsenal na Manchester United wote wana nia ya kumsajili winga wa Roma, Cengiz Under, 22, huku winga huyo wa Uturuki akipangiwa kuwa na gharama ya pauni milioni 27. (Corriere dello Sport, via Mail)

CoutinhoHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Bayern Munich imekubali kuendeleza mkataba wa makubaliano ya mkopo ya mchezaji wa Brazil, Philippe Coutinho, 28, kutoka Barcelona hata zaidi ya Juni 30, ili mchezaji huyo aweze kucheza michuano ya mwisho ya msimu huu wa Ligi ya Mabingwa Agosti. (Sky Germany, via Mirror)

Everton inaonekana kuwa tayari kutomsajili Gabriel Magalhaes, 22, kutoka Lille wakati mlinzi huyo wa Brazil akiwa amepangiwa kujiunga na upande wa Italia, Napoli. (Footmercato, via Mail)

Everton iko yatari kumsajili mlinzi wa Korea Kusini Kim Min-jae, 23, ambaye thamani yake ni pauni milioni 13.5 kulingana na Ligi ya Kuu ya China Beijing Guoan. (Guardian)

Sean DycheHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Kocha wa Burnley Sean Dyche amekosoa klabu hiyo kwa kutotatua masuala ya baadhi ya wachezaji huku mikataba ya wachezaji watano katika kikosi chake ikiwa inakamilika Juni 30. (Telegraph)

Kiungo wa kati wa Brazil, 35, Fernandinho, ambaye mkataba wake na Manchester City unamalizaika 2021, amesema kuwa angependa kufikia tamati ya taaluma yake nyumbani. (Gazeta do Povo, via Manchester Evening News)

Post a Comment

0 Comments