Kiungo mshambuliaji Shiza Kichuya ametangaza hali yah baada ya kufunga bao la kwanza tangu kusajiliwa na Simba dirisha dogo.
"Wakati najiunga na Simba kwa mara ya pili, nilikuwa sijacheza mechi za ushindani kwa zaidi ya miezi sita, hii kiuchezaji ina athari kubwa, hivyo niliomba wanipe muda, nashukuru kwa wale walionielewa na hata wale walioshindwa kunielewa nawashukuru pia kwa sababu maneno yao yalinitia hasira ya kufanya kitu.
"Sasa rasmi nimerejea katika ushindani na changamoto zote ndani ya Simba, nitaipigania timu yangu kwa kushirikiana na wenzangu hadi pale itakapotimiza malengo iliyojiwekea, nina uwezo huo na nina uhakika kila shabiki anajua nitapokuwa sawa nakuwa katika kiwango gani."
0 Comments