BETI NASI UTAJIRIKE

SAMATTA WAFUNGE HAO CHELSEA MSISHUKE DARAJA



Mbwana Ally samatta leo hii anakibarua kizito kuiongoza timu yake ya Aston villa dhidi ya Chelsea mchezo wa ligi kuu utakaopigwa leo jioni majira ya saa 12 na robo saa za Africa mashariki 

Mchezo huo utapigwa dimba la Villa Park na ni muhimu kwa timu zote kushinda kwani Chelsea yupo nafasi ya 4 akiwa na point 48 na anahitaji kusalia nafasi hiyo ili aweze kucheza ligi ya mabingwa ulaya kwa msimu ujao huku Aston vila wako nafasi ya 18 wakiwa na pointi 26  wakijikwamua kutoshuka daraja.


Samatta anategemewa kufanya maajabu hii leo dhidi ya Chelsea na inaweza kumfanya akapata timu bora zaid ya villa msimu ujao. Samatta amekuwa mwiba mkali kwa vigogo wa Uingereza baada ya kuwahi kuwafunga Liverpool msimu wa 2018/19 kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa ulaya alipokuwa akiitumikia KRC Genk lakini pia aliwahi kuifunga Manchester City kwenye fainali za Carling cup msimu wa 2019/20 . Swali ni je leo anakwenda kuwafunga Chelsea?

Mbali na Mchezo huo lakini pia Kuna michezo mingine ya EPL


Post a Comment

0 Comments