BETI NASI UTAJIRIKE

RONALDO ATAKA MBAPPE ASAJILIWE, AMKATAA HAALAND NDANI YA MADRID


Kylian Mbappe anaonekana kumuumiza kichwa mmiliki wa klabu ya Real Valladolid Ronaldo Nazario. Mmiliki huyo amesema kama bajeti yake ingekuwa sawa na Real madrid basi chaguo la kwanza kusajili nai Mfaransa Kylian Mbappe.

Kauli hiyo ya nyota wa zamani wa Real Madrid imepingwa vikali na mkurugenzi wa michezo wa PSG Bw.Leonardo kwa kusema mchezaji huyo na Neymar kwa sasa hawauzwi. Ronaldo De Lima amekuwa akimzungumzia Mbappe mara kwa mara kwa uwezo wake huku msimu huu akifunga mabao 18 kwenye michezo 20 kabla ligi hyo kusimama na baadaye kukatishwa . 

Ronaldo alinukuliwa" Kama Real Vallladolid ingekuwa na bajeti ya Real Madrid tungemsajili Mbappe,nimchezaji anayenikumbusha jinsi niivyokuwa nacheza enzi zangu"

Mkongwe huyo alimkataa Haaland kutua Real Madrid na alisema" Haaland ni mchezaji kijana, mwenye mabao mengi na huu ni mwaka wake ila tutaona mwisho wake,Ni kweli vilabu vikubwa vinamtazama lakini Real Madrid wana Benzema anayefunga mabao kila Jumapili

Post a Comment

0 Comments