RONALDO ARUDI UWANJANI KIBABE JUVENTUS IKISHINDA 2-0


Mshambuliaji wa Real Madrid ameendeleza ubabe wa kutikisa nyavu za wapinzani wake wa Serie A baada ya hii leo kufunga bao lake la 22 kwa msimu wa 2019/20. Ronaldo alikuwa wa kwanza kufungua nyavu za Bologna kwa mkwaju wa penati dakika ya 23 huku Dybala akishindilia ushindi kwa bao maridadi dakika ya 36. Mpaka kiindi cha kwanza kinamalizika Juve walikuwa mbele kwa mabao 2-0 .

Kipindi cha pili timu zote zilikamiana lakini hakukupatikana goli huku beki Danilo alieingia kipindi cha pili akipigigwa kadi dakika za nyongeza. Maokeo hayo yanaifanya Juventus kubaki kileleni mwa Serie A ikiwa na pointi 66 kwenye michezo 27 waliyocheza.


Post a Comment

0 Comments