BETI NASI UTAJIRIKE

ROMELU LUKAKU AENDELEA KUTESA MABEKI WA SERIE A INTER IKISHINDA


Ligi kuu nchini Italia imerejea rasmi hapo jana na moja ya michezo iliyokuwa ikisubiriwa kwa hmu ni ule wa Inter Millan dhidi ya Sampdoria uliomalizika kwa Inter kushinda 2-1. Inter walikuwa wa kwanza kupata goli kupitia Romelu Lukaku dakika ya 10 tu na baadaye Laurato Martine akifunga bao la pili dakika ya 33. 

Sampdoria walirudi kwa kasi kipindi cha pili na walipata bao la kufutia machozi kupitia Thorsby dakika ya 62. Matokeo hayo yanawafanya Intermilan kufikisha pointi 57 kwenye michezo 26 waliyocheza huku Sampdoria wakibaki na pointi 26 kwenye michezo 26 na kukamata nafas ya 16 kwenye msimamo wa ligi

Kwa upande wa michezo mingine ni klabu ya Atlanta kuibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi y Sassuolo .Matokeo hayo yanaifanya Atlanta kufikisha pointi 51 wakiwa nafasi ya 4 huku Sassuolo wakiwa na pointi 32 kwenye michezo 26 na wanabaki nafasi ya 12

Post a Comment

0 Comments