BETI NASI UTAJIRIKE

REAL MADRID YAZIDI KUIWINDA BARCELONA UBINGWA LA LIGA


Klabu ya Real Madrid yazidi kuikaribia Barcelona kuelekea ubingwa wa La Liga 2019/2020 .Madrid wameendelea kushika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Eibar mchezo uliopigwa dimba la Bernabeu usiku huu . 

Kiungo Toni Kroos alikuwa wa kwanza kuipa Madrid bao la kuongoza dakika ya 4 tu ya mchezo huku beki Sergio Ramos akifunga bao la pili dakika ya 30 na Marcelo akifunga bao la 3 dakika ya 37 ya mchezo. 

Matokeo hayo yaawafanya Real Madrid kufikisha pointi 59 nyuma ya Barcelona kwa pointi mbili huku wote wakicheza michezo 28 .

Kwa upande wa Atletico Madrid wao wameshindwa kutamba baada ya kulazimishwa sare ya mabao 1-1 dhidi ya Athletic Club na matokeo hayo yanawafanya kufikisha pointi 46 kwenye michezo 28 waliyocheza.

Post a Comment

0 Comments