Karim Benzema alikuwa kwenye ubora wake baada ya kufunga mabao dakika ya 61 na 86 huku Asensio akifunga bao moja dakika ya 74.Madrid walikuwa imara kuandia eneo la ulinzi kwa kuruhusu mashuti mawili tu kulenga golini kati ya 6 yaliyopigwa na Valencia.
Eneo la kiungo lilimilikiwa vyema na Casemiro ,Modric na Kroos na kuwafanya kuutawala mchezo kwa asilimia 59 dhidi ya 41 za Valencia . Eneo la ushambuliaji likiongozwa na Benzema ,Valverde/Asensio na Hazard/Vinicius lilikuwa imara baada ya kupiga mashuti 19 huku 16 yakilenga golini kwa Valencia.
Kikosi cha Real Madrid kiliongozwa na Coritous,Carvajal,Ramos,Varane ,F.Mendy,Kroos,Modric,Casemiro,Hazard/Vinicius,Valverde/Asenso na Benzema
Valencia:Cillesen,Wass,Mangala,Guillamon,Gaya,Pajero,Torres,Kondobia,soler,Rodrigo na Gomez
0 Comments