advertise with us

ADVERTISE HERE

NINI MAONI YAKO ADHABU ALIYOPEWA LAMINE MORO BAADA YA KUOMBA MSAMAHA

Uongozi wa Yanga umempa adhabu ya kulipa faini ya Tsh 1000,000 beki wa timu hiyo Lamine Moro kutokana na tukio la kumpiga teke Mwinyi Kazimoto kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara dhidi ya JKT Tanzania uliopigwa hapo jana  uwanja wa jamhuri Dodoma .


Mchezaji huyo aliomba radhi na alinukuliwa akisema 

Habari, Naitwa Lamine Morro mchezaji wa Yanga SC. .Naomba radhi kwa kitendo kisichocha kiungwana nilichokionyesha leo dhidi ya mchezaji wa JKT Tanzania. . naomba shirikisho la michezo Tanzania mnisamehe pia niliongea na mchezaji husika nikamuomba msamaha. .Naombeni mnisamehe sana kiukweli damu ilikuwa imechemka nikashindwa ku control hisia zangu nikawa over reacted. . wanachama, wapenzi wote wa soka, shirikisho (TFF) ,klabu yangu, naombeni mnisamehe haitojirudia"Lamine Morro.

Mbali na mchezaji huyo kuomba msamaa lakini uongozi wa Yanga ulikasirishwa na tukio hilo na wakamuadhibu nyota huyo 

Hii hapa ni barua iliyotolewa na uongozi wa Yanga 


Post a Comment

0 Comments