BETI NASI UTAJIRIKE

MKUDE KUKOSA MICHEZO MITATU MUHIMU YA LIGI KUU



Kiungo mkabaji wa klabu ya Simba Jonas Mkude atakosa mchezo wa jumapili dhid ya Ruvu Shooting,Mwadui na ule wa Mbeya City jijini Mbeya kutokana na majeraha.

Mkude aliumia kwenye mchezo wa kirafiki wakati Simba ilipomenyana na KMC uwanja wa Mo Simba Arena na alikimbizwa hospitali kabla ya mchezo huo kumalizika.

Awali ilidhaniwa mkude atakuwa fit kwa mchezo wa jumapili dhidi ya Ruvu shooting lakini taarifa za madaktari zinasema atakaa nje y uwanja kwa wiki mbili hivyo atakosa michezo dhidi ya Ruvu shooting ,Mwadui,Mbeya city na ule wa Prisons.

Sisi Amospoti tunamtakia kila laheri nyota huyo aweze kurejea uwanjani mapema 

Post a Comment

0 Comments