BETI NASI UTAJIRIKE

MKATABA WA PASCAL WAWA WAIBUA UTATA NDANI YA SIMBA


Beki Pascal Wawa wa Simba, maisha yake kwenye klabu hiyo yapo mbioni kumalizika ambapo suala la mkataba wake mpya limezua jambo ndani ya klabu hiyo.

Jambo ambalo limetokea kwenye mkataba mpya wa Wawa ni kujitokeza kwa makundi mawili ambapo moja linamtaka beki huyo abakishwe na kupewa mwaka mmoja huku lingine likitaka aachwe kutokana na umri kumtupa.

Taarifa zinaeleza kuwa, hali hiyo ndiyo ambayo imefanya hadi sasa beki huyo asipewe mkataba mpya licha ya ule wa awali ambao anao ukitarajiwa kumalizika baada ya ligi kufikia ukingoni.

Hivyo ndiyo hali ilivyo kwa sasa, kuna makundi mawili ambayo yote yapo juu ya mkataba wa Wawa. Kuna wengine wanataka aongezewe mwaka mmoja zaidi kwa sababu ya uwezo ambao ameuonyesha hadi sasa katika kuisaidia timu na pia kwenye mechi za kimataifa kwa msimu ujao.

“Lakini kundi lingine linabisha kwamba asipewe kwa sababu ya umri kuwa mkubwa, wanataka kuona wanatafutwa mabeki wengine wachanga ambao watapewa nafasi yake.

“Hali hiyo ya kuvutana ndiyo ambayo inafanya hadi sasa uone suala la beki huyo kupewa mkataba mpya kuendelea kuchelewa licha ya kwamba muda ambao umebaki kwenye mkataba wake ni mdogo sana,” kilisema chanzo hicho.

Post a Comment

0 Comments