Messi amekuwa nguzo kuu kwa ufungaji ndani ya klabu ya Barcelona lakini pia ndiye mfungaji bora muda wote wa La Liga akiwa na mabao 439. Bao la ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Club Depotivo Leganes linaifanya Barcelona kuendelea kukaa kileleni mwa La Liga ikiwa na pointi 64 kwenye michezo 29 dhidi ya 59 za Real Madrid waliocheza michezo 28.
0 Comments