MASHABIKI YANGA: HATUMTAKI YIKPE,AONDOKE KLABUNI KWETU


Mashabiki wa klabu ya Yanga wameonyesha hasira zao baada ya kutoka sare ya bila kufungana dhidi ya Azam FC mchezo uliopigwa dimba la taifa jjini Dar es salaam. Mara baada ya mchezo kuisha mashabiki hao walivamia basi la klabu hiyo wakisisitiza kutomtaka mchezaji wa klabu hiyo raia wa Ivory Coast Yikpe.

Mshambuliaji huyo amekuwa na wakati mgumu msimu huu baada ya kusajiliwa dirisha dogo huku akishiindwa kuonyesha thamani ya jezi ya yanga kwa kufunga magoli kwenye mechi mbalimbali. Si yeye tu lakini mshambuliaji mwenzake raia wa Congo David Molinga amekuwa akishutumiwa na mashabiki wa klabu ya Yanga kwa kutokuwa makini kwenye ufungaji.
Post a Comment

0 Comments