BETI NASI UTAJIRIKE

MASHABIKI SIMBA WAJA NA STAILI MPYA KUELEKEA MECHI NA RUVU SHOOTING


Mashabiki wa klabu ya Simba wameonekana kutilia mkazo wa Afya kuelekea mechi na Ruvu shooting mchezo utakaopigwa uwanja wa taifa siku ya jumapili 

Mashabiki wa simba wametengeneza video maalumu kwa kila shabiki atakayetaka kufika uwanja wa taifa kutazama mchezo huo . Video hiyo imeelezea hatua kwa hatua kuanzia kuingia uwanjani kisha ,mahali pa kukaa na namna ya kushangilia wakati wa mchezo.

Lengo la video hiyo ni kuwakumbusha wadau wa soka kuhusiana na janga la Corona na jinsi ya kuzuia maambukizi mapya hasa kwa sehemu za mikusanyiko ikiwemo viwanja vya soka .
Ligi kuu ilisimama mwezi machi kutokana na mlipiko wa janga la corona na sasa  inarejea rasmi kuanzia hapo kesho.

Hivi ndivyo mashabiki watapaswa kufanya kwa mechi zote za ligi

Post a Comment

0 Comments