BETI NASI UTAJIRIKE

MASAU BWILE APIGWA NA JUMA KASEJA


Msemaji wa Ruvu shooting masau bwile amepigwa na butwaa baada ya timu yake kufungwa mabao 2-1 na KMC timu inayoongozwa na kapteni Juma kaseja. Mchezo huo wa ligi uliopigwa hapo jana dimba la Chamazi jijini Dar es salaam na kuibua hisia miongoni mwa mashabiki wa soka nchini.

KMC walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia Charles Iranfya aliefumania nyavu dakika ya 29 na mpaka kipindi cha pilii kinamalizika KMC walikuwa mbele kwa bao 1-0. 
Kipindi cha pili mchezaji wa Ruvu Shooting Graham Naftal aliipa timu yake bao la kusawazish kabla Emanuel Myevukule hajafunga bao dakika ya 65 na kuufanya mchezo huo kumalizika kwa KMC 2 na Ruvu Shooting 1

Matokeo hayo yanaifanya KMC kufikisha pointi 36 wakiwa nafasi ya 12 nyuma ya Ruvu shooting wenye pointi 40 wakiwa nafasi ya 11.

Post a Comment

0 Comments