Martial anakuwa mchezaji wa kwanza wa Manchester United kufunga Hat trick ndani ya Premier League tangu kuondoka kwa Alex Ferguson mwaka 2013. Mchezaji wa mwisho kufunga Hat trick kabla ya Martial ni Robin Van Persie mwaka 2013 dhidi ya Aston Villa.
Msimu wa 2019/20 umekuwa bora zaidi kwa Martial baada ya kufunga mabao 14 kwenye michezo 25 aliyocheza tangu kusajiliwa kwake mwaka 2015 akitokea Monaco ya Ufaransa.
0 Comments