Wakati Jurgen Klopp alipowasili katika uwanja wa anfield siku yake ya kwanza kama meneja wa Liverpool tarehe 8 Okt oba 2015, kulikuwa na ujumbe mmoja katika potuba yake.
''Ni sharti tubadilike na kuamini badala ya kuwa na hofu'', alisema raia huyo wa Ujerumani huku akiwa ameketi mbele ya kamera na mbele ya ulimwengu wa wanahabari duniani.
Chini ya miaka mitano baadaye, hakuna aliye na wasiwasi na Klopp ama wachezaji wake. Baada ya kupanda kutoka nafasi ya 10 alipowasili na kuwa mabingwa wa Ulaya kwa mara ya sita, sasa pia ni mabingwa wa ligi ya premia nyumbani.
Liverpool na meneja wao walilazimika kusubiri kwa miezi mitatu zaidi ili kutawazwa kuwa mabingwa wa ligi baada ya msimu huu kusitishwa kutona na mlipuko wa virusi vya corona.
lakini taji hilo ni malipo ya jinsi alivyoimarisha klabu hiyo na mashabiki wake.
Klopp ni mtu wa kimo kirefu, mwenye uwezo wa kufunza na tabasamu. Uwepo wake katika safu ya kiufundi unafurahiwa na wachezaji pamoja na mashabiki.
Mengi hufanyika nyuma ya pazia - kuhusu jinsi anavyoangazia soka, pamoja na weruvu wake wa kutambua mbinu za kisasa zinazomfanya yeye kuonekana kama chanzo kikuu cha kuimarika kwa timu ya liverpool.
Dhana kwamba yeye hutembea katika eneo la Melwood akitabasamu na kuwakumbatia raia inaweza kuwafurahisha wale wasiopenda ufanisi wake lakini ukweli ni tofauti
Klopp anaamini uwanja wa mazoezi ndio pale ambapo tofauti huonekana. Hapa ndipo ambapo majaribio hufanywa na pale ambapo mbinu za kiufundi hujaribiwa. Tumia wazo hilo pamoja na usajili wa wachezaji bora utafanikiwa kushinda taji la ligi 2019-20 Premia.
Kila kipindi cha mazoezi hufanyiwa mipango maalum na wafanyakazi kabla ya mazoezi. Klopp baadaye atawahutubia wachezaji wake ili kuwaelezea kuhusu mpango wake kwa kina. Sio tu meneja wa Liverpool, Ni kocha mkuu wa Liverpool.
Kila kitu anachofanya kila siku kinapangwa na kuchambuliwa kwa maelezo ya dakika moja. Katika maandalizi ya mechi, hukusanya habari na kutoa uamuzi wa haraka.
Ndani ya uwanja wa Anfield - hicho kinaonekana kama kipaji muhimu ambacho kinasaidia kuelezea uwezo wake - hatua ya kufanya uamuzi kwa haraka bila kubabaika na kufanikiwa katika maamuzi hayo.
Klopp binafsi hutarajia wengine kujipanga na kuwa na utendakazi wa hali ya juu kama yeye mwenyewe. Yeye hupendelea wachezaji wake kufika kwa wakati, kila kitu kikifanyika kwa saa.
Iwapo mkutano umepangiwa kufanyika saa nne asubuhi...ni sharti ufanyike wakati huo. Ufanisi wake na Liverpool unatokana na utendakazi wa kiwango cha juu. Bidii ya mkufunzi huyo na wote nyuma yake.
Kama anavyosema: Naishi asilimia 100 kwasababu ya vijana hawa na vijana hawa. Klopp ni kiongozi, mwenye mkakati na msukumo. Lakini kwa kweli kuna timu nyuma yake.
Krawietz anaendesha timu ya wachambuzi wanne, wakizingatia masuala yote ya mechi zilizopita na zijazo - jukumu ambalo linajumuisha vipindi vya mazoezi na uteuzi wa timu. Yeye yuko kwenye uwanja wa mazoezi kila siku.
Mfano wa jinsi ushirikiano wa Klopp-Krawietz unafanya kazi huonekana katika ujumbe uliosambazwa kati ya wawili hao wakati kombe la dunia la 2018 nchini Urusi.
Walijinoa kuhusu ushawishi unaoongezeka wa kutumia mipira ya adhabu, katika safu ya ulinzi na ile ya mashambulizi, na uamuzi wa kuwa wabunifu ulitolewa, hususan wakati ambapo Liverpool ina silaha ya urefu wa beki Virgil vam Dijk na uwasilishaji wa Trent Alexander- Arnold. Ukweli haifichiki.
Katika msimu wa 2017-18, Liverpool ilifunga magoli 13 na kufungwa 12 kupitia mipira ya adhabu. Kufuatia ubunifu uliopatikana baada ya kombe la dunia , walifanikiwa kufunga magoli 29 na kufungwa manane katika kampeni hiyo.
Kampeni hiyo iliimarishwa zaidi kufuatia kuwasili kwa kocha wa kurusha mipira, raia wa Denmark Thomas Gronnemark, baada ya michuano ya kombe la dunia kama usajili uliolenga kuondoa makosa na kutumia fursa inayotolewa na mipira hiyo wakati wa mechi.
Hatahivyo Liverpool na Krawietz sio watumwa. Yeye na Klopp wanahitaji uhuru wa kufikiria na kuamua binafsi kuhusu kupiga mipira ya adhabu.
Mfano mzuri ni kona ya Trent Alexander-Arnold iliopigwa kwa haraka na kuiwacha timu ya Barcelona ikiwa imezubaa katika mechi ya nusu fainali ya pili ya kombe la klabu bingwa katika uwanja wa Anfield.
Kawaida, Krawieltz humpatia Klopp maelezo ya uchambuzi wa dakika 90 ambayo hupunguzwa na kufikia dakika 25-30 wakati wa mkutano wao wao wawili ambao mkufunzi huyo hutoa kabla ya mechi.
Lengo maalum la mkutano huo ni kwamba wachezaji wa Liverpool wanapaswa kuelezewa kuhusu uwezo wa wapinzani wao. Hatahivyo pia nao hujipatia fursa ya imani walio nayo kufanya uharibifu katika safu ya upinzani.
Klopp hatahivyo ndie anayetoa uamuzi wa mwisho. Lakini uchambuzi unaotolewa na Krawietz umekuwa muhimu mara kwa mara kama ushauri wa moja kwa moja wa kifundi unaotolewa na Lijinders.
Lijnders aliwasili katika klabu ya Liverpool mwaka 2014, wakati Brendan Rodgers alipokuwa mkufunzi. Ni msemaji , ambaye uhusika sana katika mazoezi pamoja na Klopp.
Yeye pia ndie kiunganishi kati ya idara zisizohusika na kandanda katika klabu ya Liverpool , akiangazia operesheni na kupanga muda wa kuhakikisha kuwa wachezaji wanapumzika vizuri na kuamua wakati gani wa kufanya mazoezi na kutumia fursa iliopo kushinda.
Imani ya Klopp kibinafsi na wale wanaomzunguka humfanya kusema: Najua mimi ni mzuri katika baadhi ya vitu na mzuri sana katika vitu vichache na hilo linatosha.
''Imani yangu ni kubwa mno hatua ambayo ninaweza kuwafanya watu kukua karibu nami. Hilo sio tatizo, nahitaji wataalamu karibu yangu''.
Uwanjani Klopp amejipatia umaarufu pamoja na makocha wengine wa ligi ya Premia kama vile Pep Guardiola, Carlo Ancelotti katika klabu ya Everton na Jose Mourinho katika klabu ya Tottenham.
Amefanikiwa kuwaboresha wachezaji - wale aliowasajili na wale aliowapata katika klabu hiyo.
0 Comments