advertise with us

ADVERTISE HERE

LIVERPOOL KAMA SIMBA TU BADO MECHI MOJA WAWE MABINGWA


Klabu ya Liverpool imebakiwa na mchezo mmoja tu iweze kutangazwa mabingwa wapya wa ligi kuu Uingereza kwa msimu wa 2019/20 . Liverpool  watalazimika kushinda mchezo dhidi ya Manchester City utakaopigwa tarehe 2 Julai dimba la Etihad lakini pia wanawezekana kutangazwa mabingwa mapema endapo tu Manchester City watafungwa leo kwenye  mchezo dhidi ya Chelsea.

Ushindi wa mabao 4-0 walioupata Liverpool dhidi ya Crystal palace unawafanya wajiweke mazingira mazuri ya kutwaa ubingwa huo na kuvunja mwiko wa kutoshinda kikombe hicho kwa miaka 30 mfululizo.

Kwenye mchezo huo uiopigwa dimba la Anfield uliishuhudia Liverpool wakicheza kwa kujituma huku Trent Anorld akiwa wa kwanza kufungua nyavu za Crystal Palace dakika ya 23, Mohammed Salah akipiga bao la pili dakika ya 44,Fabinho dakika ya 55 na Sadio Mane akifunga bao dakika ya 69 .

Matokeo hayo yanawafanya Liverpool kubaki kileleni kwa pointi 86 kwenye michezo 31 waliyocheza huku wakimuacha Manchester City kwa pointi 23 baada ya kucheza michezo 30.

Post a Comment

0 Comments