Liverpool imevunja mwiko uliodumu kwa miaka 30 baada ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Uingereza kwa mara ya kwanza tangu kuanza kwa mfumo mpya mwaka 1991. Liverpool wameweka rekodi ya kipekee baada ya kucheza michezo 31 na kushinda 28 wakitoka sare 2 na kufungwa mechi 1 huku wakitimiza pointi 86 na kuifanya timu hiyo kutwaa ubingwa wa EPL kwa tofauti ya pointi 23 wakiwa wamebakiwa na mechi 7 mkononi.
Kipigo cha mabao 2-1 walichokitoa Chelsea kwa Manchester City kiliifanya Liverpool kutwaa ubingwa huo kwa mara ya 19 tangu ianze kucheza EPL na kuendelea kubaki nafasi ya 2 nyuma ya Manchester United yenye makombe 20.
Shukrani ziende kwa kila mchezaji wa klabu hiyo kwa kazi nzuri aliyoifanya kuanzia safu ya ulinzi ,kiungo na ushambuliaji.
0 Comments