advertise with us

ADVERTISE HERE

LEWANDOWSKI AWEKA REKODI MPYA BAYERN IKISHINDA 4-2


Kipute cha ligi kuu Ujerumani Bundesliga kimeendelea tena wikiendi iliyopita kwa mechi mbalimbali huku Bayern Munich wakiendelea kuusogelea ubingwa wa 2019/2020. Tukio kubwa kwa wikiendi hii ni Robert Lewandowski kufunga bao lake la 30 kwenye mechi 30 za Bundesliga alizocheza msimu huu. 

Bayern Munich waliibuka na ushindi wa mabao 4-2  dhidi ya Bayern Leverkusen na kuwafanya waweze kufikisha pointi  70 kwenye michezo 30 waliyocheza.Mchezo kati ya Bayern Leverkusena na Bayern Munich uliopigwa dimba la BayArena huku Alario akifunga bao la kuongoza dakika 10 za mchezo lakini Coman alisawazisha dakika ya 27, Goretzka akifunga bao la 3 dakika 42, Gnabry dakika ya 45. 

Mpaka mapumziko Bayern alikuwa akiongoza kwa mabao 3-1 . Dakika ya 66 Lewandowski alifunga bao la nne kwa upande wa Bayern Munich huku Wirtz akifunga bao la 3 kwa Bayern Leverkusen dakika ya 89. mchezo huo ulipigwa bila mashabiki na Bayern Munich wamekuwa na wastani wa kufunga mabao 3 kila mechi na wastani wa kufungwa bao 1 kila mechi.

Post a Comment

0 Comments