Barcelona anatakiwa kushinda mchezo huo ili kurejea kileleni baada ya Real Madrid kushinda mechi dhidi ya Espanyol na kuwafaya waongoze ligi kwa pointi 71 dhidi ya 69 za Barcelona.
Endapo Barcelona atafungwa mchezo huo basi atakuwa na kibarua kigumu kutwaa La Liga kwa msimu huu kutokana na uchache wa mechi zilizobaki. Atletico Madrid na yeye anakazi ya ziada kwa kushinda mchezo dhidi ya Barcelona ali aendelee kubaki nafasi ya 3.
Lionel Messi atakuwa na kazi moja tu ya kufunga bao lake la 700 tangu alipoanza kucheza soka la kulipwa.
0 Comments