BETI NASI UTAJIRIKE

KAULI YA HAJI MANARA MANARA BAADA YA KUTWAA UBINGWA WA LIGI KUU


Afisa Habari wa klabu ya Simba Haji Sunday Manara amefurahishwa na ubingwa wa ligi kuu Tanzania Bara kwa mara ya tatu mfululizo kwa Klabu yake ya Simba. Manara alisafiri mpaka jijini Mbeya kuutazama mchezo wa igi kuu kati ya Simba na Prisons uliomalizika kwa sare ya0-0. Kupitia mitandao yake ya kijamii manara aliipongeza timu hiyo na kuwashukuru mshabiki huku akiahidi kushinda mataji mengine 7 mfululizo.

"Ubingwa huu ni kwenu Washabiki wetu kokote mlipo, nyie ndio mnalostahili pongezi za kwanza,nyie ndio Mastar wetu, kwangu binafsi naona bila nyie tusingekuwa Machampioni,,mmetupa hanikizo kokote tulipokwenda,,mmetupa ujasiri hata tulipokuwa dhaifu,mmetupa kila aina ya hamasa, nitawaomba uongozi wa klabu wafanye yafuatayo, kwa kuwa kikombe hiki ni chetu hadi kiyama, tukitoe kama zawadi kwenu.hongereni sana 🙏🙏
Hashtag yetu #badomakombesaba

Post a Comment

0 Comments