KAGERA SUGAR WAKO FITI KUWAKABILI YANGAKagera Sugar hii leo wana kazi ya kupambana na Klabu ya Yanga kwenye mchezo wa hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho.Mchezo huo utapigwa majira ya saa 1:00 usiku unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na kila timu kuhitaji kusonga mbele.

Kocha Mkuu wa Kagera Sugar, Mecky Maxime amesema kuwa mpango mkubwa nikupata matokeo ili kusonga mbele kwenye hatua ya nusu fainali.

Maxime ataingia uwanjani akiwa na kumbukukumbu ya kuwanyoosha Azam FC kwenye mchezo wa ligi uliochezwa Uwanja wa Kaitaba kwa bao 1-0.

Yanga nao pia mchezo wao wa mwisho wa ligi Uwanja wa Taifa iliibuka na ushindi wa mabao 3-2 mbele ya Ndanda FC.

Kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza kwenye ligi walipokutana Yanga na Kagera Sugar Uwanja wa Uhuru, Kagera Sugar iliibuka na ushindi wa mabao 3-0.

Ulikuwa ni mchezo wa kwanza kwa Kocha Mkuu, Luc Eymael kukaa kwenye benchi la ufundi ndani ya Yanga akichukua mikoba ya Luc Eymael.

Eymael amesema kuwa yupo tayari kwa ajili ya kupambana na Kagera Sugar kwani wachezaji wana morali kubwa. Mshindi wa mchezo wa kesho atakutana na mshindi wa mchezo kati ya Simba na Azam FC.

Post a Comment

0 Comments