BETI NASI UTAJIRIKE

JOHN BOCCO ,MOHAMED HUSEIN WAZUA GUMZO YANGA ,WATAJWA KIKOSINI


Mshambuliaji wa Yanga Deus Kaseke amepanga kikosi chake cha kwanza ambacho anaamini kitampa ushindi ndani ya dakika 90.Kwenye kosi hilo la kazi yeye pia amejipa namba kwa kuwa anaamini anastahili kuwa ndani ya kikosi hicho.


Amewabeba nyota wawili pekee kutoka Simba na kuwapa namba ndani ya kosi lake la kazi huku akimpa jukumu la kufunga mabao mshkaji wake Ngassa.


Hiki hapa kikosi cha Kaseke:-
 
Kipa atakuwa Metacha Mnata wa Yanga.


Beki wa kulia atakuwa Juma Abdul wa Yanga.


Beki wa kushoto Mohamed Hussein wa Simba.


Beki wa kati atakuwa Kelvin Yondani wa Yanga

Beki wa kulia atakuwa Lamine Moro wa Yanga

Kiungo mkabaji atakuwa Papy Tshishimbi wa Yanga.

Winga atakuwa Deus Kaseke mwenyewe wa Yanga.

Kiungo wa kati atakuwa Haruna Niyonzima wa Yanga

Mshambuliaji atakuwa John Bocco wa Simba

Mshambuliaji Mrisho Ngassa wa Yanga


Winga atakuwa Bernard Morrison wa Yanga

Post a Comment

0 Comments